Muda na maeneo ya ya viwanja vitakavyotumika bado havijatangazwa rasmi ila Mji utakaofanyika michuano hii ni mji maarufu wa PRAGUE.
FFT inapenda kushiriki michuano hii kwa kupeleka mabingwa wa Tanzania iwapo kutakapopatikana nafasi za ushiriki, na hata kama FFT ikikosa nafasi ya ushiriki basi itawapeleka baadhi ya mabingwa na viongozi wa FFT kwenda kuangalia namna gani michuano hiyo hufanyika.
"Tunaomba wadau na wapenzi wa mchezo huu kujitokeza kwa wingi katika kudhamini na kufadhili safari hii maana Safari hii ni safari yetu sote, tunakumbuka mwaka jana tulishindwa kwenda kutokana kwa kuchelewa kupata taarifa na tukashindwa kujipanga vizuri juu ya safari hii, lakini tulifanya jitihada za kumuona Waziri wenye dhamana na alitutia moyo kutuambia hata kama tukishindwa kwenda 2016 basi tujipange mapema kwa ajili ya 2017 na tangu hapo mwishoni mwa mwaka jana tulianza mipango na mikakati na hivi sasa tumeanza kujipanaga rasmi juu ya safari" - alisema Kaimu Msaidizi wa Msemaji Mkuu wa FFT.
Pia "Tunajipanga kuanzisha kampeni kwa ajili ya safari ya kwenda kwenye michuano hiyo na tupo katika uchaguzi wa jina la kampeni ambalo mpaka sasa 'TWENZETU 'SUPERBALL', Safari hii ni yetu sote' limeonekana kupata kura nyingi japo bado majina yanaendelea kupokelewa na kuingizwa katika kinyang'anyiro cha jina bora la kampeni. Nia na madhumuni ya kampeni hii ni mengi mengi mno" - alisema Kaimu Msaidizi wa Msemaji Mkuu wa FFT. .