NEYMAR JR’S FIVE OF TANZANIA
Mpira wa Miguu wa Vigoli Vidogo
UTAMBULISHO
Neymar Jr’s Five ni mashindano / michuano ya mpira wa miguu wa vigoli vidogo unaochezwa na wachezaji watano watano kwenye mechi kwa kila timu / kikosi. Timu / kikosi kamili huwa na wachezaji saba, wachezaji wawili waliongezeka ni wa akiba. Wachezaji wanaoshiriki michuano ya ngazi kubwa huwa wana umri miaka 16 - 25. Kwenye mechi, timu itakayofungwa goli mchezaji wake hutoka / hutolewa. Mechi huchezeshwa kwa dakika 10 tu hivyo basi, timu itakayotoa wachezaji wake wote 5 kabla ya muda wa mechi kuisha / kumalizika itakuwa imepoteza USHINDI vilevile kila timu ikiwa imebaki na mchezaji mmoja mmoja katika funga nikufunge basi mchezaji atakayefunga goli litaitwa GOLI LA DHAHABU na MFUNGAJI WA DHAHABU. Wachezaji huvaa BIBS zenye nembo ya NEYMAR JR’S FIVE kwa mbele na nyuma zenye namba kubwa kwa juu kuanzia #.1 hadi #.7 na chini yake huwa na maandishi “OUTPLAY THEM ALL”.
FAINALI YA MICHUANO YA DUNIA
Fainali ya kwanza ya michuano ya dunia ilikuwa 2016 nchini Brazil ambayo iliwakutanisha wachezaji 65,000 kutoka mataifa 47. Fainali ya pili ni 2017 Julai 7 - 8 Santos, Brazil kwenye viwanja vya Taasis ya NEYMAR JR (Instituto Neymar JR) ambavyo viliwakutanisha wachezaji 104,228 kutoka mataifa 53 ya mabara 6. Kwa upande wa bara letu la Afrika zilishiriki mataifa 5 kwa hatua ya makundi na kufikia hatua ya nusu fainali ni taifa 1 kama ifuatavyo:-
1. NIGERIA
2. SOUTH AFRICA
3. ANGOLA
4. MISRI
5. MAURITUS
Hatua ya 32 bora ni NIGERIA, SOUTH AFRICA, MISRI, ANGOLA. Angola 5 – 0 Azerbaijan
Hatua ya 16 bora ni ANGOLA, 2 – 0 Ukraine
Hatua ya 8 bora ANGOLA, 3 – 1 Bosnia
Hatua ya 4 bora ANGOLA, 0 – 1 ENGLAND
Hivyo basi, kwenye viwango vipya vya NEYMAR JR”S FIVE vya AFRIKA, timu inayoongoza ni ANGOLA, NIGERIA, SOUTH AFRICA, NA MISRI.
SAFARI YA ROMANIA YA KUTWAA UBINGWA
Hatua ya makundi, Romania ilikuwa KUNDI B
NAFASI KUNDINI - II
MICHEZO - 5
MAGOLI - Shinda 15, Fungwa 4
Alama - 9
Hatua ya 32 bora, 5 – 1 Jordan
Hatua ya 16 bora, 1 – 0 Italy
Hatua ya 8 bora, 5 – 0 Kosovo
Hatua ya 4 bora, 4 – 0 Sweden
Hatua ya 2 bora, 1 – 0 England
Idadi ya magoli yote ya kufunga 31 na kufungwa 5 kwenye michezo 10.
NEYMAR JR’S FIVE YA TANZANIA
Inaendeshwa na kusimamiwa na FREESTYLE FOOTBALL of TANZANIA (Uchezeaji wa Mpira wa Miguu wa Tanzania – FFT) kwa kushirikiana na Redbull Tanzania na Shadaka Sports Management. Wameanza mipango na mikakati ya kuandaa michuano hii kwa ngazi zote kuanzia chini kwenda juu ili mwaka 2018 ipeleke timu ya kwenda kuiwakilisha taifa letu pindi itakapotangazwa michuano hii. Hivyo basi, Afisa mtendaji mkuu ambaye ni Rais wa FFT ndugu Morison Mosses amewataka kwa wale mashabiki wa NEYMAR JR wajitokeze kushiriki michuano kwa kuunda timu zenye wachezaji 7 wenye umri 16 – 25 wakiongozwa na viongozi 3 (Kocha / Meneja / Benchi la ufundi). Nafasi za ushiriki wa timu zitatangazwa wakati wowote hivyo zikitangazwa kiongozi wa timu atawasilisha majina 7 ya wachezaji na 3 ya viongozi wa timu.