Genius MP

Nembo rasmi ya Genius MP
Ni klabu mama ya mchezo wa kuchezea mpira wa miguu yenye jukumu na mamlaka ya kusimamia, kuendesha na kuratibu mchezo huu. Ilianzishwa 2015 na kusajiliwa Aprili 27, 2016 kwa kupewa namba ya usajili NSC 11410. Klabu ina uhusiano na shirikisho la  ulimwengu ambalo balozi wake mkubwa ni Ronaldinho Gaucho. Waanzilishi ni Morison Mosses na Pascal Chang’a.

MADHUMUNI
(a) Kupiga vita aina zote za ukatili wa kijinsia na uvunjaji wa haki za wachezeaji mpira.
(b) Uwepo wa mashindano ya kata, wilaya, kanda, mkoa, kitaifa na mataifa na ya mashirika ya umma na binafsi.
(c) Kujenga uwezo kwa kutoa elimu katika masuala ya elimu ya mchezo.

(d) Kutetea na kushawishi uboreshaji wa miundo mbinu na huduma za mchezo katika ngazi mbalimbali.
(e) Kuwezesha upatikanaji wa fursa mbalimbali za kimaendeleo na kushawishi wachezeaji kujiunga katika vikundi  mitandao mbalimbali yenye manufaa kwa wachezeaji.
(f) Kuhakikisha ukuaji wa soko la mchezo linakuwa kubwa.
(g) Kuifanya sekta ya michezo kukua kiuchumi.
(h) Kuwepo kwa ajira kwa waendeshaji na wachezeaji mpira.

MAJUKUMU
(a) Kuandaa, kusimamia na kuendesha mashindano ya kata, wilaya, kanda, mikoa, kitaifa na mataifa kwa ujumla.
(b) Kutangaza Sheria, Taratibu na Kanuni za mchezo - STK.
(c) Kufanya jitihada za kushiriki mashindano ya kimataifa na Ulimwenguni.
(d) Kushauri na kutoa mafunzo ya utaalamu wa utengenezaji wa miundo mbinu ya mchezo ulio bora.
(e) Kuandaa, kusimamia na kushauri kuhusu program za ushauri nasaha.
(f) Kuvumbua vipaji vya kuchezea mpira.

MAMLAKA
(a) Kuhakikisha mchezeaji ana uhuru wa kupata haki za binadamu za msingi.
(b) Kuhakikisha tunashiriki mashindano ya kimataifa na Ulimwenguni.
(c) Kudumisha uhusiano wa kirafiki na mataifa jirani, Afrika kwa ujumla na Ulimwenguni kote.
(d) Kusajili wachezeaji, waendeshaji, vilabu, na mashindano n.k.


MIPANGO NA MIKAKATI
(a) Mipango na mikakati ya muda mfupi kila mwaka itakuwa;
(i) Kutafuta na kuibua vipaji; haya ni mashindano ambayo yatafanyika mikoani na baadhi yatakuwa yanaooneshwa kwenye runinga. Mashindano haya yataitwa FFTS (FREESTYLE FOOTBALL TALENT SEARCH).
(ii) Kuandaa shindano kubwa la Ubingwa; hili ni shindano la kitaifa ambalo litakutanisha mabingwa wa kuchezea mpira wa miguu Tanzania kutoka sehemu mbalimbali za mashindano waliyoshiriki. Shindano litaitwa TFFC (TANZANIAN FREESTYLE FOOTBALL CHAMPIONSHIP).
(iii) Maandalizi ya siku ya kuchezea mpira duniani itakayoadhimishwa tarehe 1 Septemba kila mwaka na inaweza kuwa siku ya utoaji tuzo kuu za kuchezea mpira zitakazoitwa FFT Awards (FREESTYLE FOOTBALL TANZANIA AWARDS).
(b) Mipango na mikakati ya muda mrefu kila mwaka itakuwa;
(i) Matayarisho ya kujenga kiwanja cha mchezo.
(ii) Maandalizi ya kuwa na shindano la dunia lije kufanyika nchini kwetu.

Nifanyaje kuomba

U A N A C H A M A - G e n i u s MP
Jaza fomu ya uanachama, kisha ipeleke Ngome kuu, ofisi ya klabu ya Genius MP, kamati ya usajili.

U B I A

U S H I R I K A

U D H A M I N I

U F A D H I L I

Ruksa Fursa kuwa:

1. Mchezeaji mpira
2. Kocha
3. Jaji
4. MC
5. Mtawala / Kiongozi / Mtumishi