Neno la Rais

FFT yazindua blog mpya.

Ndugu wapenzi na wadau wa uchezeaji / kuchezea mpira wa miguu Tanzania. Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu muweza wa yote. Ni jambo la heshima na fahari kwa FFT yetu kuweza kuwa na blog ya kisasa kama hii. Ndugu msomaji ninakushukuru kwa kuitembelea. Ndugu zangu, hii blog ni yetu sisi sote, tuitumie kwa kupashana habari, kuelemishana na pia kuburudishana kwa mikanda mbalimbali mifupi ya matukio ya michezo itakayokuwa inawekwa hapa.

Blog hii itakuwa ni chombo chenu cha kuwapeni wasomaji fursa ya kujua nini kinaendelea FFT, na pia kuwapeni fursa ya kuchangia maendeleo ya uchezeaji / kuchezea mpira wetu kwa kutoa ushauri na maoni mbalimbali. Changamoto ni jambo la kawaida viongozi kukutana nazo, hivyo wadau wa uchezeaji mpira msisite kutukosoa pale mnapoona hatuendi vizuri. Kikubwa ni staha, tukosoane, tuelimishane kwa staha.

Ninapenda nigusie mambo machache yaliyoko mbele yetu yanayohusiana na maendeleo ya uchezeaji mpira wetu. Kama mnavyofahamu kote duniani, chimbuko la maendeleo ya uchezeaji / kuchezea mpira wa miguu iwe ni ngazi ya vilabu au ngazi ya timu za Taifa ni uwekezaji katika uchezeaji mpira wa watoto na vijana. Kwa hapa nchini kwetu tunatarajia kuanza mashindano ya mikoa ili kumtafuta bingwa wa Tanzania. Baadae kwenda kupeleka timu ya taifa nchi ya Jamhuri ya Czech katika shindano la ubingwa wazi la dunia la uchezeaji mpira wa miguu liitwalo "Superball" tarehe 20-26 Agosti, 2017.

Kwa kushirkiana na serikali, wadau na familia ya uchezeaji / kuchezea mpira wa miguu nchini ninaamini tutafanikiwa katika kuandaa michuano hiyo ya mikoa kwa watu wenye uwezo wa kuuchezea mpira.

Vilevile kuja kwa ujio wa viongozi wa shirikisho la dunia la uchezeaji mpira wa miguu WF3 (World Freestyle Football Federation) pia tunataraji ujio wa balozi mkuu wa dunia wa mchezo huu Ronaldinho Gaucho.

Nitumie fursa hii kuyaomba makampuni, taasisi, na mashirika mbalimbali kujitokeza kudhamini / kufadhili programu hizo.

FFT - "Sanaa Ya Soka. Burudani Tosha".

Nifanyaje kuomba

U A N A C H A M A - G e n i u s MP
Jaza fomu ya uanachama, kisha ipeleke Ngome kuu, ofisi ya klabu ya Genius MP, kamati ya usajili.

U B I A

U S H I R I K A

U D H A M I N I

U F A D H I L I

Ruksa Fursa kuwa:

1. Mchezeaji mpira
2. Kocha
3. Jaji
4. MC
5. Mtawala / Kiongozi / Mtumishi