Leo Idara ya utumishi na utawala bora ya Ngome kuu - Ofisi ya Rais imemtunuku cheti cha mtumishi bora wa mwezi wa Januari Makamu wa Rais ndugu Pascal Chang'a kwa kujituma vya kutosha katika kutekeleza majukumu na wajibu wa uchezeaji wa mpira kwenye kila ngazi ijapokuwa ni wajibu wake kufanya hivyo ila ameonesha ufanisi mkubwa katika kukaimu Ofisi nyingi za kurugenzi kama ilivyo kwa Rais wa uchezeaji wa mpira wa miguu Tanzania ndugu Morison Mosses naye kufanya vizuri pia.
CHETI CHA MTUMISHI BORA
Cheti hiko ni ishara ya kuhamasisha watumishi wengine kufanya shughuli zao kwa ufanisi mkubwa zaidi. Cheti hiko ndicho cha kwanza kutolewa na ofisi ya Rais na pia kurugenzi zote. Cheti cha mtumishi bora kitakuwa kinatolewa kila baada ya mwezi na inapendelewa kutolewa kila ofisi ya kurugenzi ya uchezeaji mpira wa miguu Tanzania.
Sifa za kutunukiwa Cheti.
1. Amekuwa mtii kwa maagizo ya Rais.
2. Amekuwa mbunifu wa utendaji kazi (kujiongeza).
3. Amekuwa Kaimu mzuri wa Ofisi za kurugenzi mbalimbali.
4. Amekuwa kiongozi bora kwenye kamati mbalimbali alizoteuliwa na kuchaguliwa.
5. Amekuwa muwezeshaji kifedha katika kuendesha Ofisi mbalimbali za uchezeaji wa mpira.
Sifa za utunukiwaji wa cheti bado zinaendelea / zitaendelea kutolewa au kuvumbuliwa kila siku kila mwezi kwenye kila Ofisi ya Uchezeaji mpira wa miguu ili kuleta uthamani na ubora wa cheti.
Dira ya utoaji wa cheti
Kuleta hamasa kubwa ya kutumikia vyema na zaidi uchezeaji wa mpira wa miguu.
Dhamira ya utoaji wa cheti
Kuleta ushindani mkubwa wa utumishi.
Uthamani wa Cheti unaotakiwa baadae
Cheti hiko kitakuwa kinatolewa na zawadi nyingine kama vile fedha, vitendea kazi n.k
Imetolewa na:
Kitengo cha utoaji vyeti
Idara ya utumishi na utawala bora
Ofisi ya Rais - Ngome Kuu
Mtoaji:
Kaimu Mkuu wa Idara ya utumishi na utawala bora - ngome kuu.